Ngoba anaingia kwenye mchezo hatari! Akiwa na mke wa Kamishna (na pia mpenzi wake wa siri), wanapanga na kutekeleza wizi wa pesa kwenye kasino bila wasiwasi. Wakati huo huo, mambo yanazidi kuwaka nyumbani — Mqhele anapigana na kaka yake Khosa, Nkosana anaingia kwenye majukumu mapya kama mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wa teksi, na Hlomu anakutana na aliyekuwa mpenzi wake. Je, hii ni mwanzo wa vurugu kubwa zaidi kwenye familia hii? Usikose The Wife ndani ya Maisha Magic Bongo!