Watoto wa amanzi wachoshwa na tabia za baba yao kumpiga mama yao kila mara. Mmoja wa watoto wake (Kombo) analipuka kwa hasira na kumuelekezea bastola – ni tukio la kushtua, lenye hisia nzito na mshangao kwa kila anayeshuhudia. Baada ya tukio hilo Amanzi anatumbwa rumande na huko anakutana na kichapo kutoka kwa wafungwa wenzie.
JIVU linaendelea kuvunja ukimya kuhusu dhuluma za kifamilia na maamuzi yanayobeba maumivu makubwa.