maisha magic bongo logo

Wolper na Kadinda Ndani ya DStv

Habari
17 Aprili 2025
Joto kuelekea kuanza kwa kipindi cha TheMakeOver linazidi kupanda, Hawa hapa majaji wetu. Watakuwa ni majaji wa namna gani?
Season 1

Kipindi kipya cha The Makeover kinatua ndani ya Maisha Magic Bongo kikiwa na nguvu mpya, na majaji wake wawili — Jacqueline Wolper na Martin Kadinda — wanao leta msisimuko kwa mashabiki kabla hata ya show kuanza tarehe 25 aprili saa mbili usiku.

Wolper, msanii na fashionista maarufu, ni jina kubwa kwenye tasnia ya burudani. Uwepo wake kama jaji unaleta mvuto, uzoefu na moyo wa kuinua wengine. Martin Kadinda, mbunifu wa mavazi wa kiwango cha kimataifa, anajulikana kwa anavyozingatia ubora linapokuja suala la mitindo na ubora.

Wakiwa pamoja kwenye jopo la majaji, duo hili limeendana kwa namna ya kipekee. Lakini bado swali linaendelea kuwachanganya mashabiki:

Watakuwa majaji wa aina gani?

Watapewa nafasi ya kuonesha huruma kwa washiriki au tutarajie maamuzi ya papo kwa papo na maneno yenye utani mkali?

Kitu kimoja ni dhahiri — Wolper na Kadinda wanakuja na glam, class, na maamuzi yenye ushawishi.

The Makeover si tu kipindi cha mabadiliko ya muonekano, bali ni safari ya watu wa kawaida kupata nafasi ya kujiamini na kung’ara — mbele ya kamera na katika maisha ya kila siku.

Usikose! The Makeover inaanza Aprili 25 kwenye Maisha Magic Bongo, DStv Channel 160.