maisha magic bongo logo

"The Makeover" Kabumbu la brush na powder

Habari
11 Aprili 2025
Kuanzia Aprili 25, usikose safari hii ya kusisimua ya washiriki na timu ya wataalamu wakiongozwa na Annie Independent, Jacqueline Wolper, Martin Kadinda na Alma.
Season 1

Kwa mara ya kwanza kabisa Maisha Magic Bongo  tunawaletea kipindi kipya, chenye msisimko  na maudhui ya urembo. The Makeover ni kipindi kipya cha urembo kinachotarajiwa kuanza rasmi tarehe 25 Aprili 2025 saa 2:00 usiku.

Tangu kutangazwa rasmi, mitandao ya kijamii imetawaliwa na shauku kutoka kwa mashabiki ambao hawawezi kusubiri kuona mambo yatakwavyo kuwa kwenye runinga zao.

Kwenye ukurasa wa Instagram wa Maisha Magic Bongo, hizi hapa baadhi ya comment zao:

@iamcalypsoo let’s go Bronx 🔥🔥🔥

@smartbeautyparlor Woyooo 😍🔥

@tom7_lets goooo ⚡🔥

Kipindi hiki kitaongozwa na mtangazaji mahiri Annie Independent na kitawashirikisha majaji nguli na maarufu: Jacqueline Wolper  (msanii na fashion icon) pamoja na mbunifu wa kimataifa Martin Kadinda. Aidha, Alma, mtaalamu wa urembo, atakuwa jicho la 3 kusimamia magic zote za make-up na washiriki wote.

The Makeover inaleta zaidi ya burudani --ni jukwaa la kuinua, kujiamini, kusherehekea  urembo, na kuwapa nafasi wasanifu wachanga kung’ara kupitia usaidizi wa wataalamu.

Kama unapenda mitindo, vipodozi na hadithi zinazogusa mioyo. Usikose kuangalia The Makeover, kuanzia Aprili 25 kupitia Maisha Magic Bongo – DStv Channel 160.