maisha magic bongo logo

Tamara Amkabili Lindiwe, Nguvu Apuuza Kisa cha Mke Wake – Mpali IS5I Ep 202 – 205IMaisha Magic Bongo

Video
11 Julai

Wiki hii ndani ya Mpali, hali ya sintofahamu imetanda kwenye familia ya Nguzu. Ugomvi mkubwa unalipuka kati ya Tamara na Lindiwe, kila mmoja akitaka kusimama imara — lakini je, kuna aliye tayari kuachia nafasi? Mvutano huo unazidi kuibua migogoro mipya katika familia. Wakati huo huo, Nguvu anaketi na wake zake lakini bila kujali kuwa mmoja wao hajarejea nyumbani kwa siku mbili mfululizo. Kauli yake ya kupuuza hali hiyo inawashangaza wake wenzake — na inaibua maswali mazito juu ya uaminifu na usawa katika ndoa yao ya mitala.