Wiki hii ndani ya Huba imetawaliwa na maumivu, mshtuko na hali ya wasiwasi.
Abby ametekwa nyara, na hatma yake bado haijulikani. Kila sekunde inapita ikiwa ni mzigo kwa familia na mashabiki walioguswa na tukio hilo la kutisha.
Wakati huohuo, Nicole anakumbana na mateso mitaani baada ya kuvamiwa na wahuni waliomuibia kila kitu. Amejeruhiwa na kurejea nyumbani akiwa amejaa huzuni na hofu, akamfuata Ritha akiwa amevunjika moyo kabisa.