Julai ya kibabe ndani ya Maisha Magic BongoJulai ya Kibabe Imeanza!
Mwezi huu Maisha Magic Bongo inawasha moto wa burudani usiku na mchana! Kuanzia tamthilia mpya kama Broken Pieces, kurudi kwa vipenzi kama Huba na Mpali, hadi vichekesho vya Kitimtim, mabadiliko ya The Make Over, na muziki moto ndani ya Asumani Vibes — kila siku ni sherehe ya vipindi bora kabisa. Usikose pia filamu za Kitanzania kila wikendi, zenye visa vinavyogusa maisha halisi.
Kaa nyumbani wakati wa mvua ukitumia Maisha Magic Bongo Msimu huu wa mvua, jifunike vizuri na ufurahie season finale za tamthilia kali—Gharika na Yolanda—kwenye Maisha Magic Bongo, DStv Channel 160.
Je, haki itashinda ndani ya Gharika au wahusika watazama kwenye mafuriko ya hatima zao? Na Yolanda, ataweza kujinasua au njama zitamzamisha?
Usikose! Nje kunanyesha na kuna kibaridi, lakini ndani kuna hadithi zenye joto la burudani isiyo na kifani!