Julai ya kibabe ndani ya Maisha Magic Bongo
Julai hii, Maisha Magic Bongo inakuletea msimu wa kiwango cha hali ya juu! Kutoka kwenye tamthilia zenye mvuto, kipindi cha Urembo, vichekesho vya kukata na shoka, muziki murua hadi filamu bora za Kitanzania — mwezi huu ni wa kusisimua kwa kila mtazamaji.
Uzinduzi Mpya: Broken Pieces
Tunakuletea *Broken Pieces* — tamthilia ya Kituruki iliyotafsiriwa kwa Kiswahili. Hadithi ya familia mbili zilizoathiriwa na majanga, mapenzi, na siri nzito. Ni simulizi inayogusa moyo na kukuacha ukitamani zaidi kila usiku.
Inarushwa: Jumatatu hadi Alhamis saa 1:00 usiku
Tamthilia Zinaendelea
Huba – Sehemu ya 14
*Huba* S14 inarudi na moto mpya! Migogoro ya kifamilia, usaliti, mapenzi tata na wahusika wapya wanaongeza moto kwenye kila tukio.
Jumatatu hadi Jumatano saa 3:00 usiku
The Make Over – Hatua ya Mchujo
The Make Over imeingia hatua ya kusisimua zaidi — mchujo! Washiriki wanapambana kwa nafasi yao huku wakionyesha mabadiliko ya kuvutia.
Kila Ijumaa saa 2:00 usiku
Â
JIVU – Ghetto Lazima Lichome
*JIVU* linaendelea kufichua maisha halisi ya mtaa. Munir anaendelea kupambana na Familia yake kwa ajili ya kulinda penzi lake kwa Karen ambaye hajakubalika kwenye familia ya kina Munir kwa sababu za utofauti wa kitamaduni.
Jumatano saa 3:30 usiku
Mpali – Sehemu ya 5
Mapenzi, urithi na migogoro vinaendelea kutikisa familia ya Nguzu. Jairos anajaribu kujisafisha huku Sandra akichagua kati ya upendo na wajibu.
Jumatatu- Alhamis saa 2:00 usiku
Vichekesho: Kitimtim
*Kitimtim* inaingia katika msimu wake wa 48 na visa vya kufurahisha! Majirani, upuuzi na kejeli kali vinakupa dozi kamili ya comedy baada ya hekaheka za siku nzima.
 Jumatatu- Jumanne 3:30 Usiku
Muziki: Asumani Vibes
Ukihitaji kupumzika, washa *Asumani Vibes*. DJ Ally B anakuletea reggae tamu, singeli za kijanja na vibes laini za jioni.
Jumatatu hadi Ijumaa saa 11:00 jioni
Filamu za Wikendi
Filamu bora za Kitanzania kila wikendi! Kutoka kwenye drama nzito hadi mapenzi ya mitaani — ni hadithi zinazozungumza na maisha yetu.
🕓 Jumapili saa 2:00 usiku
Tazama Wapi
• Tazama Maisha Magic Bongo kupitia DStv Channel 160• Baadhi ya vipindi vinapatikana kwa mtiririko kupitia Showmax (kutegemea eneo).
Endelea Kufuatilia
Kwa masasisho ya kipekee, video fupi na mazungumzo na mashabiki, tufuatilie kupitia:
Instagram | Facebook | YouTube – @MaishaMagicBongo
Â